YESU NI JIBU

Jumapili, 1 Aprili 2012

KUFUNGULIWA NA KUWEKWA WAKFU KWA KANISA SAHARA SPIRITUAL CENTER

Maaskofu na wachungaji wametakiwa kutumia mtandao kutangaza na kuhubiri neno la Mungu pamoja na kutoa taarifa ya makanisa yao.

Kauli hiyo imetolewa na askofu mkuu wa Tanzania Assemblies of God askofu Barnabas Mtokambali wakati wa ufunguzi wa kanisa la Mabibo Sahara TAG lililopo mabibo jijini Dar es saalam linaloongozwa na askofu wa jimbo la kaskazini mashariki askofu Geoffrey Massawe.

Akizungumza katika ufunguzi huo askofu Mtokambali alisema kuwa ni vema kila kiongozi wa kanisa kutumia mtandao kutangaza kanisa lake pamoja na neno la Mungu maana wewe wanasaidika pale mchungaji anapohubiri neno la Mungu katika mtandao na kuongeza kuwa ni njia mojawapo ya kiuinjilisti.

Aidha aliongeza kuwa kiongozi wa kanisa anpoweka na namba ya simu katika mtandao inasaidia maana kuwa watu wanakuwa na mahitaji mbalimbali hivyo anapiga simu kwa mchungaji akiwa na uhitaji hivyo mchungaji anapata nafasi ya kumwaombea.

Akisoma risala mkungaji kiongozi wa kanisa hilo askofu Massawe alisema kuwa kanisa hilo mpaka kukamilika limegharimu fedha kiasi cha milioni120 kwa awamu ya kwanza na katika awamu ya pili ya upanuzi wa kanisa hilo litagharimu kiasi cha milioni sabini.

Hata hivyo aliongeza kuwa kutakuwepo na awamu nyingine ya ujenzi wa jengo kubwa kwa lengo la kuwafikia watu wengi zaidi na kuwepo mahali pazuri pa kumwabudia Mungu.

Pamoja na hayo kulikuwepo na changamoto mbalimbali ila hazikukwamisha kufanya kazi ya uinjilisti,kuwepo kwa kanisa dogo bado tuliweza kufanya mikutano mbalimbali katika sehemu mbalimbali kama vile Malolo Mozi ,Mamba Kibondo,Mwipenge Musoma,IgowoleMfindi,Bugando Bukoba,Kibeche Mheza,Ludewa Iringa,Kawona Kilindi na Mhoro Rufiji na tnategemea kufanya mikutano mwaka huu wa2012 katika maeneo ya Mchukwi Rufiji,Kimara na Chalinze alisema askofu Massawe.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni