YESU NI JIBU

Jumatano, 25 Aprili 2012

KUTEMBELEA KWA MWINJILISTI WA KIMATAIFA JOHANES AMRIZA KATIKA KANISA LA DCT

Imeelezwa kuwa ili mkristo aweze kuishi maisha ya ushindi na yenye mafanikio siku zote lazima amtegemee Mungu (Yesu) sambamba na kufanya maombi kuwa ni sehemu ya maisha yakena atakuwa mtu wa ushindi.

Kauli hiyo imetolewa na mkurungezi wa huduma ya SOS mwinjilisti Johanes Amriza katika kanisa la Dar es salaam Calvary Temple liloko Tabata shule .
Kanisa hilo linaongozwa na mchungaji Ron Swai ambaye pia ni katibu mkuu wa kanisa  la Tanzania Assemblies of God.

 Kutokana na hilo ni vema basi waumini wa kristo kukaa chini ya uongozi wa Roho mtakatifu na kujifunza jinsi ya kumtumikia Mungu katika roho na kweli na kumwabudu yeye pekee yake maana ndiye mwenye uwezo.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni