Chanzo cha nguvu ya
Mungu na uwepo wa Roho mtakatifu ndani ya kanisa ni pale tu kanisa ulimwengu
walipojitoa katika kushirikiana na taifa la Israeli.
Kauli hiyo imetolewa
na Askofu mkuu wa huduma ya maombi na ushauri wa kibiblia (BCIC) na pia ni
msimamisi mkuu wa WAPO MISSION INTERNATIONAl Askofu Silverster Gamanywa katika
mkesha uliofanyika katika kanisa hilo siku ya ijumaa ya tarehe 27 april.
Amesema hayo wakati
akielezea lengo la ziara ya kuwaongoza waumini mbalimbali katika safari ya
kutembelea taifa la Israel ambapo ziara hiyo itakuwa mwezi wa saba mwaka huu.
Baraka za Mungu
zimetoweka katika mataifa mengi kutokana na waumini kutoshirikiana na taifa la
Israeli kusema kuwa kuna baraka za Mungu
ambazo bado zinaandamana na wana wa Israeli likiwepo baraka ya kubariki taifa
hilo nawe utabarikiwa na ukilaani taifa hilo utalaaniwa.
Kwa mkiristo halisi
lazima aunganishwe na baraka za taifa hilo maana ni makosa kutengana na taifa
hilo maana ukienda kinyume nawe wewe ni adui wa taifa hilo
Aidha Askofu
Gamanywa amesema kuwa umaskini wa taifa la Tanzania limetokana na kutokuwepo
kwa muunganiko na taifa hilo
Akielezea juu ya
gharama za kuchangia ni dola za kimarekani elfu mbinu na mia tisa ambayo ni
gharama ya tiketi ya ndege,hoteli ,chakula pamoja na nauli za usafiri za ndani wakati
wote wa ziara.
Hata hivyo ameongeza
kuwa ataongoza maombi na maombezi katika taifa hilo na kuahidi kuwa endapo watu
watakubali kutembelea taifa la Israeli watakuwa wameungana na baraka za baba wa
imani Ibrahimu.
Njia ya kuweza
kufanya ni kurejesha uhusiano na taifa
hilo pili utainuka kiuchumi maana hoteli utakazolala ni za taifa hilo na
vyakula na usafiri utakaotumika ni ya waisraeli hivyo utakuwa umechangia katika
pato la taifa hilo na kuunganishwa na baraka za taifa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni