YESU NI JIBU

Alhamisi, 3 Mei 2012

MKESHA ULIOFANYIKA BCIC MBEZI BEACH WA KUWAOMBEA MAKUNDI MAKUU MATANO

 Askofu mkuu na mwangalizi wa WAPO MISSION INTERNATIONAL askofu Silverster Gamanywa akifundisha katika mkesha uliofanyika katika kanisa la BCIC Mbezi beach .
Katika mkesha huo askofu Gamanya aliwafanyia maombi na maombezi makundi makuu matano,ambapo makundi hayo ni
  1. kundi la watu waliompokea Yesu katika maisha yao.
  2. watu waliokuwa na matatizo mbalimbali ikiwepo magonjwa.
  3. kundi la wanandoa ili Mungu awasaidie katika ndoa zao.
  4. kundi la vijana wa kike ambao hawajaolewa wala hawana wachumba.
  5. kundi la mwisho la vijana wa kiume ambao hawajaoa wala hawana wachumba.
Hata hivyo kabla askofu hajawaombea makundi hayo aliweza kuwafundi neno la Mungu nakuwashauri  baada ya hapo ndipo anawafanyia maombi na maombezi.Aliongeza kusema kuwa ni vyema kukaa chini ya uongozi wa Mungu na kutafuta kuwa mtakatifu wakati wote maana Mungu ni mwaminifu hata kuacha bila kukubariki na kukutana na mahitaji yako.
Pia amewaonya wazazi kukaa na kuwalea watoto wao na vijana wao katika njia zinazompendeza Mungu.


Askofu anatoa maelekezo kabla ya kuanza kufanya maombi.



 Hawa ni baadhi ya watu waliofika kwenye mkesha na kuombewa sala ya toba na askofu Gamanywa.




Hawa ni wanandoa waliokuwa wakiombewa kwenye mkesha mafanikio katika ndoa zao

 Hawa ni baadhi ya wasichana waliofika kwenye mkesha wanafanyiwa maombezi na wanasikiliza kwa makini maelekezo kabla hawajaanza kuombewa.






  Hawa ni waimbaji wa DGC wakitoa huduma ya uimbaji katika mkesha katika kanisa la BCIC Mbezi beach.


 Askofu Gamanywa akiwaongoza wachungaji wa BCIC katika kuombea salada iliyotolewa kanisani hapo wakati wa mkesha





Hivi ndivyo waumini walivyokuwa wakionekana wakimsikiliza kwa makini askofu Gamanya ambaye hayupo pichani wakati akifundisha neno la Mungu.






Waumini wakimwabudu Mungu katika mkesha.




 Waimbaji wa BCIC Mbezi beach wakiimba katika mkesha


Hivi ndivyo madhabahu ya BCIC inavyoonekana.







Hakuna maoni :

Chapisha Maoni