YESU NI JIBU

Jumapili, 19 Februari 2023

LIJUE KUSUDI LA MUNGU KUKUOKOA NA KUKUACHA ULIMWENGUNI.

 

ASKOFU ZAKARIA OSWARD RULE AKIFUNDISHA KATIKA KANISA LA JSF SOMO LA KUTAMBUA KUSUDI LA MUNGU KUKUOKOA NA UMEACHWA ULIMWENGUNI.

Kila mwamini ameokolewa na kuendelea kuishi ulimwenguni ilikutimiza kusudi la Mungu kwa muda wote atakaoishi.Hayo yamebainishwa na mchungaji Zakaria Osward Rule wa kanisa la Jesus Save Fellowship (JSF)lilopo karakata Dar es salaam wakati akifundisha katika ibada ya jumapili.

   Aidha askofu Rule alisema kuwa kila mwamini anapookoka anapewa jukumu la kufanya kwa muda wote akiwa ulimwenguni.

  Alinukuu kitabu cha yohana 17:11-19 ambapoalisema kuwa Bwana Yesu aliwaombea wale waliomwamini,

 Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.

   Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.

 Na sasa naja kwako; na maneno haya nayasema ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao.

Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.

Aliongeza kuwa Yesu alisema kuwa Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu.Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.

Askofu Rule alifafanua mstari wa 17 kuwa Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.

Mwamini yeyote anapookoka hutakaswa na neno la Mungu ambalo litakuwa ndani ya maisha yake ya kila siku ya wokovu.

"Pasipo neno hakuna mwamini yeyote mwenye nguvu ya kuushinda ulimwengu na anasa zake,maana kuna vishawishi ambavyo ni neno pekee ndilo lenye uwezo wa kusaidia kuushinda"alisema.

Yesu aliwapa waliomjia uwezo na nguvu ya kuiendea ulimwengu na kuwafanya wanaulimwengu kuwa wanafunzi wa Bwana Yesu kama yohana 17:18 inavyoelezea Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni. Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.

Hata hivyo askofu Rule alisisitiza waumini kutenga muda wa kujifunza neno la Mungu maana linaleta hekima,kuongeza maarifa na kuwa na nguvu ya kuushinda ulimwengu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni