YESU NI JIBU

Ijumaa, 30 Oktoba 2015

SHEREHE YA KUMKABIDHI HATI YA USHINDI YA URAIS DR JOHN POMBE MAGUFULI NA MGOMBEA MWENZA SAMIA SULUHU KATIKA UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE JIJINI DAR ES SALAAM.

Zoezi la kukabidi hati ya  ushindi kwa mshindi wa chama cha mapinduzi ccm ndugu John pombe magufuli na mgombea mwenza limefanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini DSM ambapo mwenyekiti wa tume ya uchaguzi NEC jaji mstaafu wa mahakama ya Rufaa Damian Lubuva amesema kuwa katiba ya tanzania inampa tume kibali ya kutangaza mgombea ambaye amekuwa na kura nyingi kuliko wagombea wenzake.
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva (kulia), akimkabidhi hati ya ushindi ya Urais, Rais Mteule wa Tanzania Dk.John Magufuli katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam leo. Kushoto ni Makamu wa Rais Mteule, Samia Hassan Suluhu.
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva (kulia), akimkabidhi cheti cha Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu katika hafla hiyo.
Rais Mteule wa Tanzania, Dk. John Magufuli (kulia), akiwapungia mkono wananchi wakati wa hafla hiyo ya kukabidhiwa cheti cha urais. Kutoka  kushoto ni mgombea urais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira na mgombea nafasi hiyo kupitia Chama cha ADC, Chief Lutalosa Yemba.
  Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo.
   Rais Mteule wa Tanzania, Dk.Magufuli akimuonesha Rais Jakaya Kikwete hati ya ushindi.
 Rais Mteule wa Tanzania, Dk.Makufuli akiwa katika picha ya pamoja na wagombea urais wenzake wa vyama vingine.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpongeza Mwenyekiti wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian 
Lubuva kwa kusimamia vizuri uchaguzi mkuu wa 2015.
Rais Jakaya Kikwete na Rais Mteule Dk.John Pombe Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja na wake zao kwenye hafla hiyo.

Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi (kushoto), akimpongeza 
Rais Mteule wa Tanzania Dk. John Magufuli baada ya kuchaguliwa kuwa rais.
Makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakishangilia wakati Rais Mteule wa Tanzania Dk.John Magufuli alipokuwa akitoka Ukumbi wa Diamond Jubilee kukabidhiwa cheti cha urais. 
picha kwa hisa mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni