YESU NI JIBU

Jumamosi, 5 Oktoba 2013

SEMINA YA WANANDOA IMEFANA KATIKA UKUMBI WA BCIC MBEZI BEACH.

Semina ya wanandoa imekuwa ya furaha sana pale ambapo kila kundi limeweza kupewa fursa na nafasi ya kupata maelekezo juu ya matatizo yanayotakana na ndoa.

Akifundisha katika semina hiyo ambayo imehudhuriwa na  wachungaji .viongozi mbalimbali wa siasa na serikali pamoja na waumini wa madhehebu na dini mbalimbali askofu Sylvester Gamanywa alisema kuwa ndoa si taasisi ya mtu binafsi bali ya Mungu mwenyewe ndiye mwasisi wake.

Ndoa ni muunganiko wa watu wawili ambao wamekubaliana kuishi pamoja na kudhamiria kuwa pamoja,na wakati akifundisha alisema kuwa kuna chero saba zinazo sababisha ndoa kuvunjika.

Hata hivyo askofu Gamanywa alisema kuwa ni vyema kuwepo na mapatano ya kina ndani ya ndoa na kuwepo kwa maamuzi ya pamoja,wala mwanaume asiamue mwenyewe na wala mwanamke asiamue pekee.

 Askofu Silvester Gamanywa akianza kufundisha wanandoa ambao wamefika katika semina ya wanandoa.

 Mafundisho yakiendelea.


 Wakati wa kusifu na kuabudu kabla ya semina kuanza katika ukumbi wa BCIC Mbezi Beach




 Washiriki wa semina ya wanandoa hapo juu wakimsifu na kumwabuddu Mungu kabla semina haijaanza. 

Upendo Kilahiro akiabudisha na kuimbisha katika semina ya wanandoa kusifu na kuabudu.

 








 Askofu Gamanywa akifundisha katika seminaya wanandoa.






Washiriki wa semina ya wanandoa wakifuatilia kwa makini semina ya wanandoa .

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni