YESU NI JIBU

Jumanne, 24 Septemba 2013

KUJARIBIWA SIO DHAMBI,DHAMBI NI KUANGUKA MAJARIBUNI:

  KUMTUMKIA MUNGU NA KUSHINDA MAJARIBU:

Imeelezwa kuwa suala la kumtumikia Mungu na kumwabudu ni la mwanadamu mwenyewe ambaye amejitakasa na kuacha njia zake mbaya,na hapo pia atawepata baraka zake za kiungu pale atakapo tii na kufuata sheria na taratibu za Mungu.

hayo yalinenwa na mchungaji Peace Mazinde kutoka Mombasa kenya wakati akifundisha katika kanisa la Mabibo Sahara TAG katika ibada ya jumapili ambapo alikuwa akihitimisha semina ya wiki moja iliyoendeshwa kanisani hapo.

Aidha alisema kuwa hapo Yesu alipokuwa duniani hajaomba kili waumini ama wafuasi wake wasiingie majaribuni ila aliomba ili washinde majaribu na kuwapa tuzo wale wanaoshinda majaribu,ambapo aliongeza  kuwa, kujaribiwa  sio dhambi, dhambi ni kuanguka majaribuni,

Akinukuu kitabu cha 2 nyakati 15:1-2 alisema kuwa kuna mambo matati ambayo muumini anatakiwa kuyafuata na kuzingatia katika maisha yake ya ukristo siku zote na hapo ataweza kuwa mwamini mzuri wa kristo.

ya kwanza ni kujitakasa,pili ,kunyenyekea na tatu ni kujiachia kwa Bwana na ukifuata hayo kama mwamini utamp-endeza Mungu alisema,

na kwa ujuma alisema jukumu la kutunza wokovu wako ni lako mwenyewe sio la kiongozi wako wa dini sio askofu mchungaji mwinjilisti wala nani ni lako mwenyewe. 

   Hapa mchungaji Peace Mawinde akifundisha katika ibada.mchungaji Mazinde akihubiri neno kanisani.

 

 

 

;

Mchungaji kiongozi wa kanisa la Sahara Mabibo TAG askofu Jofrey Masawe akihimiza jambo kwa waumini hawapo pichani katika ibada ya jumapili

Mke wa Askofu Masawe mchungaji OLiver Masawe mfupi akiwa na Atho Dave ambaye anaishi Australia na familia yake alipotembelea kanisani hapo.

 Kikundi cha kusifu na kuabudu wakihudumu madhabahuni.

Waumini wakimsifu na kumshangilia Mungu katika ibada ya kusifu na kuabudu.






Hakuna maoni :

Chapisha Maoni