YESU NI JIBU

Jumanne, 6 Agosti 2013

MCHAWI ASALIMISA VIFAA VYA KICHAWI KANISANI EAGT CITY CENTER

Wakati wiki 13 za ujesho zikitimia mganga na mchawi maarufu amesalimisha vifaa vyake vya kichawi katika kanisa la EAGT katika viwanja vya mwalimu julias Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam.
Akizungumza kanisani hapo mganga huyo ambaye amefahamika kwa jina na Steve Mgaya amesema amekuwa akitumika katika sehemu mbalimbali kwa kufanya uchawi na uganga ambapo ameweza kufanya wengi walokimbilia kwake kupanda vyeo katika kazi na maofisini mwao.
Aidha bwana Mgaya ameongeza kuwa amekuwa akifanya uchawi kwa muda mrefu maana uchawi aliyokuwa nayo ni wa kurithi kwenye familia yake na amekuwa akitumia kwa muda wote kwa kuwaangamiza watu mbalimbali kuwatupia mikosi nuksi na mabalaa mbalimbali  hadi hapo alipojisalimisha kwa Yesu.

Akielezea jinsi alivyojisalimisha kwa Yesu bwana Mgaya alisema kuwa aliwalogo hata na watoto wake na hata mke wake wa kwanza aliweza kumuua kwa njia ya kichawi jambo ambalo ni la kusikitisa sana wachawi wanavyowafanyia wanadamu wenzao.

"Kiukweli mkwe wangu alikuwa anaumwa na mguu kwa muda mrefu na ndipo alipo niomba nimsindikize ili aje aombewe na mchungaji Florrian Katunzi,na nipoamua kuongozana naye tulipofika karibu na geti la kuingilia chuo cha utalii na bandari nilianza kuhisi kuwa naishiwa na nguvu huku walinzi wangu wakiniacha mmoja baada ya mwingine ,"alisema ndugu Mgaya
Kiukweli Yesu yupo maana mara baada ya kuingia na kukaa mchungaji alipoanza kufundisha na kuita watu wa kuja kutubu nimekuwa wa kwanza kukimbia mbele na dakika chache sijaelewa kilichoendelea,baada ya hapo nilijikuta nimezungukwa na watu wengi huku nikiwa chini ,kwa kusema kweli nilikasirika sana ila ashukuriwe Mungu maana ni mwema sana hata nami kaninona sasa ni mwaminifu sana 


 Huyu ndiyo Steven Mgaya  ambaye amesalimisha zana zake za kichawi

 Hapa anaelezea jinsi alivyokutana na bwana Yesu

 Anasimulia huku mchungaji Katunzi ambaye amevaa suti nyeusi akimsisitiza 


 Akionesha baadi ya vifaa vya kichawi

 Anaishika na kuonesha juu ni pembe ambazo hutumika kwa kulia watu

 Hiyo ndiyo pembe yenyewe 

 Vijiti vilivyofungwa na kamba ni zindito ambayo alikuwa akitumia bwana Mgaya kuzindika magari yake.

 Sime hiyo ilikuwa ikitumika kukatakata nyama za watu ambayo hutumika kuwalisha misukule.


Hapa juu ni zana za kichawi alizokuwa akitumia bwana Mgaya.

 Mke wa bwana Mgaya akielezea jinsi alivypona mguu.

 Hapa anafurahia baada ya kushuhudia.

 Mchungaji Katunzi akimwombea mtoto ambaye alikuwa atolewe kafara.

 Hapa ni mama mzazi wa mtoto ambaye alikuwa atolewe kafara

 waumini wakiombea familia ya bwana Mgaya

 Mama mzazi wa kichanga akiombewa na mchungaji Katunzi

 mke wa bwana Mgaya akiombewa


 hapa naye bwana Mgaya hakuwa nyuma kuombewa


Maoni 1 :

. alisema ...

kama ungependa kuokoa uhusiano/ndoa yako basi nitakupendekeza kwa Dk Dawn. alinisaidia kurejesha nyumba yangu baada ya miezi 11 ya utengano mkali kati yangu na mume wangu. Nilielekezwa kwake na dada yangu mkubwa wakati ndoa imeisha, akarudisha amani na furaha katika ndoa yangu, pia amesaidia marafiki zangu wengine na wanaishi kwa furaha kwa msaada wa Dk Dawn,
Wasiliana naye ikiwa unahitaji usaidizi wa kurejesha uhusiano/ndoa yako/ ikiwa unataka kupata mimba au kuponya aina yoyote ya ugonjwa:
Dk Dawn hatawahi kukukatisha tamaa:
Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com
WhatsApp: +2349046229159

Chapisha Maoni