YESU NI JIBU

Jumatatu, 19 Agosti 2013

ATAKAYELIBARIKI TAIFA LA ISRAELI,ATABARIKIWA ,UNGANA NA ASKOFU GAMANYWA KWA ZIARA YA KINABII NCHINI ISRAELI.



Msomaji nakualika kufuatilia  makala  maalum ya  ziara ya kinabii nchini Israeli, ambapo jopo la Watanzania kesho linaondoka kulekea nchini Israeli, kwa ajili ya kutembelea maeneo matakaifu, kujifunza zaidi Biblia  na kufanya maombi.Ziara hii ya Kinabii ni Maono ya Askofu Mkuu Sylivester Gamanywa wa WAPO MISSION INTERNATIONAl, ili kuwasogeza  Watanzania kuijua zaidi Biblia na mafunuo yake,  na hivyo kuvuna baraka za Mungu, ambazo zimeahidiwa kwa wote watakaojifungamanisha na taifa hilo la Israeli.
Wanaziara hao watakaa nchini Israeli kwa muda wa siku kumi za kazi nzito ya kutembelea maeneo matakatifu, kujifunza Biblia na kufanya maombi.


Msomaji, kumbuka Ziara nyingine ya Kinabii kama hii, inatarajiwa kufanyika tarehe za mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka huu. Unachotakiwa kufanya hivi sasa ni kujiandaa kwa kuanza kulipa fedha katika benki ya CRDB nambari 02J1080000700, inayopokea  dola za Kimarekani pekee.

Akaunti hiyo imefunguliwa kwa ajili ya watu wanaotaka kushiriki katika Ziara za Kinabii nchini Israeli zinazoandaliwa na WAPO MISSION INTERNATIONAL. Kwa anayetaka kushiriki anaweza kuanza kulipa fedha kidogokidogo au kwa mkupuo dola za  Kimarekani 3000 tu. Baada ya kufanya malipo, tunza risiti yako na uwasilishe kopi yake,  kwa mratibu wa ziara Elibariki Minja, anayepatikana katika ofisi za WAPO Radio FM Kurasini Jijini Dar es Salaam. Nambari za simu za Mratibu wa Ziara Bwana Elibariki Minja ni 0786205768, 0715 452730 na 0754 452730.
Unaweza kuwasiliana naye sasa kwa maelekezo zaidi.

Kumbuka katika ziara ya Kinabii ya mwezi Desemba, ofa maalum ya kuwasafirisha bure watumishi wanaochunga makanisa itatolewa kwa kigezo maalum! Hivyo changamkia sasa ofa hiyo ili nawe uzuru Israeli ambako ndiko hasa kwenye chimbuko la imani yako, hususan wewe Mkristo  anayemkiri Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako.

Msomaji,hebu sasa tunayaangalie maeneo matakatifu  yatakayotembelewa, ikiwa ni mfululizo wa maeneo hayo, ambayo tulianza kuyachambua tangu wiki iliyopita.

Eneo ambalo Yesu alibariki mikate mitano na samaki wa wawili  na kulisha maelfu ya watu, nalo litatembelewa na Wanaziara ya Kinabii  kutoka nchini Tanzania, ambao  wanaondoka kesho jioni.Ikizungumzia tukio hilo   katika Injili ya Luka 9: 14,  Biblia inaeleza kuwa:.. akaitwaa ile mikate mitano   na wale samaki wawili,  akatazama juu mbinguni  akavibariki, akavimega, akawapa  wanafunzi wake  ili waandikie mkutano.  Wakala, wakashiba wote; na katika vile vipande  vilivyobakia, walikusanya vikapu kumi na viwili. Watu waliokula walipata kama  elfu tano..(Luka 9:14)
Katika Mathayo 14:15 – 21 Biblia inabainisha kuwa nao waliokula walikuwa wanaume wapata elfu tano, bila wanawake na watoto.Eneo jingine litakalotembelewa na Wanaziara ya Kinabii kutoka nchini Tanzania ni Mlima wa Heri.Hapa ni pale ambapo kwa mujibu wa Kitabu cha Injili ya Mathayo 5:3-10, Yesu Kristo aliketi mlimani akifundisha juu ya Heri tisa.“Heri  walio masikini wa roho, maana  ufalme wa mbinguni ni wao, Heri  wenye huzuni, maana hao  watafarijika……”“Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki,  maana  ufalme wa mbinguni ni wao…”“Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno  baya kwa uongo, kwa ajili yangu, furahini na kushangilia kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni ;kwa maana ndivyo  walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yangu”.
Hizo ni baadhi ya tisa ambazo Yesu alizifundisha kwa wanafunzi wake. Wasomi wazuri wa Biblia wanazielewa sana heri hizi na mafundisho ya Injili ndani yake.Msikilizaji eneo hili ambalo linatunzwa sana ni  eneo moja zuri sana lenye bustani safi za matunda na miti ya Mizeituni. Ukoka safi na maua mengi. Mungu akusaidie siku moja nawe ufike. Tafadhali wasiliana na Mtaribu Elibariki Minja, ili uweze kushiriki katika ziara ya mwezi Desemba. Nambari zake za simu ni 0786205768, 0715 452730 na 0754 452730


Msomaji Wanaziara watapata fusra ya  kuuona Mlima Hermoni.

Wakazi wa Kanaani  yaani Waamori  walikuwa wakiuita Senir, wakati wakazi wengine wa  Sidoni waliuita Sirion  (Zaburi 29:6,  1Nyakati 5:23, Ezekieli 27:5, Kumb 3:9). Mlima Hermoni Kibiblia ni mpaka wa nchi ya ahadi yaani Kanaani, waliyahidiwa Wana wa Israeli na Mungu (Kumbu. 3:8), ( Joshua 11:17, 12:3, 13:5)

Vijito vya maji vilinavyotiririka kutoka katika Mlima Hermoni hukutana  na vingine kutoka katika mapango hayo yanayofahamika kama Panias na kuungana,  kisha kuelekea katika Mto Yordani na baadaye katika Bahari ya Galilaya.

Kitu cha msingi  katika historia ya Biblia Takatifu ni kwamba,  katika eneo hili la mlima Hermoni lenye miamba na mapango mengi, Yesu Kristo alifika na wanafunzi wake. Na ndipo alipomwambia Mtume Simon Petro kwamba atampa funguo za Ufalme wa Mbinguni na lolote atakalolifunga duniani,  litafungwa hata mbinguni.(Mathayo 16:13-20). Hapa ilikuwa baada ya Yesu kumuuliza Perto kwamba wanafunzi wake wanamnenaje.

Alipomtupia Mtume  Perto swali hilo, alimjibu kwamba anamnena kuwa  yeye ni Kristo, Mwana wa Mungu aliyehai.
 “……Heri Simon Baryona  kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali baba yangu aliye mbinguni”,  Ndivyo Yesu alivyomjibukwa mujibu wa Injili ya Mathayo 16:15-17 na Marko 8:27-30..

Msomaji  Vilele vya milima ya Golani ni sehemu muhimu kwa Israeli ya sasa. Wanaziara wa Kitanzania watapa fursa ya kuliona.


Vilele vya milima ya Golani hufahamika  kama Golan Heights kwa Kiingereza, kwa Kiebrania ni Ramat Ha Golan, wakati kwa kiarabu ni Mustafaatu I-Jawlan. Hivi ni vilele vya milima ambavyo kimsingi viko  katika pembe ya Kusini mwa  milima mingine ya Lebanoni, ambayo inaunda mpaka wa Israeli na Syria.

Hivi ndivyo vilima vilivyotwaliwa na Israeli kutoka katika milki ya Syria kunako mwaka 1967,  wakati wa Vita vya Siku Sita kati ya Mataifa ya Kiarabu na Israeli.Theluthi mbili ya milima hiyo iko chini ya Israeli, inayoishikilia kwa kiapo cha kutoiachia kamwe, hata kama ni milki ya Syria.

Umoja wa Mataifa (UN), Jumuiya ya Ulaya (EU), Uingereza, Marekani, Umoja wa nchi  za Kiarabu  na Jumuiya nyingine za Kimataifa,  zinatambua kwamba  milima hiyo  ni miliki   ya Syria ila tu Israeli imeikalia kwa nguvu.

Mwaka  1981, Israeli ilipitisha sheria ikijiruhusu kuvimiliki kisawasawa vilele vya Milima ya Golani, na kuviwekea hadhi ya umiliki  kamili, hatua ambayo ilipingwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kwa azimio nambari  497. Vilele vya Milima ya Golani vina kilomita mraba  1,800 sawa na maili mraba  690.

Kwa nini Israeli inavishikilia vilele hivi vya milima ya Golani?.

Maji na Kilimo:
Kuna vyanzo vizuri ya maji yanayoingia katika Bahari ya Galilaya. Maji kutoka katika Mlima Hermoni huingia katika Mto Yordani na kuunganika na maji mengine yanayotoka katika vilele vya Milima ya Golani,  na kumiminika katika Bahari ya Galilaya.

Katika bonde la Milima ya Golani kuna eneo zuri kwa ajili ya kilimo. Shughuli hiyo  huendeshwa katika mashamba ya Shebaa yaliyoko katika sehemu ya bonde la Mto Yordani, Milima ya Golani na Hermoni. Ni eneo leye rutuba sana na safi mno kwa kilimo na maji.

Ulinzi na usalama:
Vilele vya milima ya Golani, vinatoa  nafasi nzuri sana ya suala zima la Ulinzi kwa taifa la Israeli.Unapopanda katika vilima hivi, unayaona mataifa matatu  ya Kiarabu yanayoizunguka Israeli, mataifa hayo yate kwa namna moja au nyingine ni maadui wa Taifa  la Israeli.

Ukikaa katika kilele  kimoja kikuu cha Milima ya Golani, unakuwa kama Mfalme aliyekaa katika kiti chake cha enzi,  akiwatazama watumishi wake kwa chini. Ukiwa hapa huweza kuona Mataifa ya Lebanoni, Yordani Syria na Israeli yenyewe.Ni eneo muhimu la kivita na kiusalama kwa Israeli. Ikiwa Israeli italiachia na kulikabidhi kwa Syria, hakika Israeli itafutiliwa mbali kutoka katika ramani ya uso wa dunia. Golani ni roho ya ulinzi wa Israeli.

Msomaji, huna sababu ya kukosa kushiriki katika ziara za kinabii kama Mungu amekupa uwezo huo.Wasiliana na Mratibu Elibariki Minja, kwa ajili ya ziara ya mwezi wa kumi na mbili mwaka huu kwa simu nambari 0786205768, 0715 452730 na 0754 452730

Bahari ya chumvi,  Dead Sea, au Bahari Mfu  ni moja ya maeneo yakayotembelewa na wanaziara ya kinabii kutoka Tanzania. 

Ni Bahari yenye urefu wa Kilomita 76 na upana wa Kilomita 18, ikiwa katika eneo la Kusini Mashariki mwa taifa la Israeli.  Kwa Kiebrania Dead Sea inafahamika kama  Yam Hamelach.
Kuibuka kwa Bahari hii maelfu kwa maelfu ya miaka iliyopita, wataalam wanasema kulitokana na miamba inayounganisha Bara la Afrika na taifa la Syria, kuvunjika na kutitia.

Bonde la Mto Yordani, Bahari ya  Galilaya na Bahari ya Chumvi au Dead Sea,  vyote vinatokana na tukio hilo la kijiografia, ambalo kwa waliobobea katika maswala ya Jiografia, wana nafasi nzuri  ya kulielewa..

Bahari hii imelala katika uwanda wa jangwa la Judea,  ambalo linakutana na jangwa kubwa kabisa nchini Israeli, Jangwa la Negev.Chanzo kikuu cha maji katika Bahari ya Chumvi  ni Mto Yordani, unaotiririsha maji yake kutoka katika pembe ya Kusini ya Bahari ya Galilaya.

Dead  Sea au Bahari ya Chumvi, ndiyo inayoongoza kwa kuwa ni maji yenye chumvi nyingi kuliko bahari yoyote ile   ulimwenguni. Kiasi cha chumvi kinachopatikana katika maji ya Bahari hii,  ni mara nane ya kinachopatikana katika bahari nyingine ulimwenguni.

Kiasi hicho cha chumvi, kinaizidi chumvi inavyopatikana katika Bahari ya Mediterania mara kumi.

Takwimu zinaonesha kuwa asilimia kumi ya chumvi yote ulimwenguni inapatikana katika maji ya Bahari hii iliyokufa  au The Dead Sea.

Madini hayo yaliyoko katika maji ya Dead sea,  ni dawa nzuri ya macho kwa wenye matatizo ya macho. Wengi waliyatumia yakawasaidia, kuona vyema.Watu wengi wanaotembelea bahari hii ya chumvi, huoga katika maji yake, na kujipaka  matope mwilini, ambapo ngozi zao huwang’ara na kupona magonjwa yaliyokuwa yakizifanya zionekane zimesinyaa na kuchoka.

Katika pwani ya Bahari hii ya chumvi katika eneo liitwalo Mitzpe  Shalem karibu na Qumran kuna kiwanda kikubwa cha vipodozi. Pia kuna maduka ya bidhaa nyingine nyingi za kawaida, mahoteli, nyumba za kulala wageni na beach  za stahere mbalimbali.

Zama hizo, Malkia wa Sheba, Kushi au Ethiopia alifika katika Bahari hii na kuoga, kujipaka matope yake, akang’ara na kumeremeta sana. Mfalme Sulemani, Malkia Cleopadra na Herode the Great wote walipata huduma ya bahari hii.

Sehemu nyingine ambayo Wanazira wa Kitanzania watatembelea ni pamoja na Mji wa Kursi. Mji huu uko mashariki mwa Bahari ya  Galilaya au ziwa Genezareti, kama kilomita saba kufika njia panda ya kuelekaea katika vilele vya Milima ya Golani au Kiti cha Mfalme Israeli. Enzi za Yesu Kristo katika karne ya kwanza, Mji huo uliibuka na rekodi ya kipekee kwa mnyama aitwaye nguruwe.

Katika kitabu cha Mathayo Biblia inauelezea Mji wa Kursi kwamba ulikuwa wa nchi ya Wagerasi.Wakati mmoja Yesu akiwa katika nchi hiyo, Wagerasi  wawili wenye pepo walikutana naye.Mara wale pepo ndani yao walipomtambua Yesu walianza kulia na kupiga kelele: “Tuna nini nawe Mwana wa Mungu?, Je umekuja kututesa kabla ya muula wetu?”.

Wakati hayo yakiendelea, tazama kwa mbele kulikuwa na kundi kubwa la nguruwe likichungwa na  wachungaji. Kilichotokea ni kwamba  wale pepo walimsihi Yesu wakimwomba kama anataka kuwafukuza kutoka  ndani ya Wagaresi wale, awaruhusu  wawaingie nguruwe wale.

Yesu akawaambia nendeni. Wale pepo wakawatoka wale Wagerasi na kuwainga nguruwe wale. Maskini. Kilichofanyika hapo ni wale nguruwe wote kupagawa pepo na kukimbia hadi katika Bahari ya Galilaya  na hatimaye kuzama na kufa maji.Mji wote ulipopata habari ulitoka kwenda kumwona Yesu kwa hofu, na moja kwa moja, wakazi wa mji huo, wakamsihi aondoke mipakani mwao. (Mathayo 8:28 – 34).

Mji wa  Naini ni sehemu nyingine ambayo jopo la wanaziara ya kinabii kutoka nchini Tanzania litaitembelea.
Ni Mji uliopo karibu na Mlima Tabor (Mlima Wakubadilika Sura) uliopo Kusini Magharibi mwa Bahari ya Galilaya.Ni katika eneo la Mji huu, ambapo Yesu Kristo akiwa na wanafunzi wake na watu wengine walifika katika lango  lake na kukutana na  maiti ya mtoto pekee wa mwanamke mjane, ikipelekwa kuzikwa makaburini.

Katika Luka 7:13-15, ikielezea tukio hilo Biblia inaeleza kuwa Bwana alipomwona alimuonea huruma, akamwambia usilie,  akakaribia, akaligusa jeneza, wale waliokuwa wakilichukua wakasimama. Akasema kijana, nakuambia inuka. Yule maiti akainuka, akaketi!

Katika mji huu watu wanaotembelea Israeli, hutumia waombea wajane na watoto wao, ili wakutana na Yesu Kristo, na  kupata suluhu ya kudumu ya dhidi matatizo yao.  Kumbuka Neno la Mungu linatuambia kuwa Yesu Kristo ndiye mume wa wajane!

Msomaji, hayo ni baadhi ya maeneo yakayotembelewa  na Wanaziara ya Kinabii kutoka nchini Tanzania ambao wanaondoka kesho jioni, wakiongozwa na Askofu Sylivester Gamanywa ambaye ndiye mwandaaji Mkuu  na mbeba maono ya Ziara hizo za Baraka.

Ufanye mwaka huu wa 2013 kuwa wa baraka za kipekee kwako kwa kushiriki katika Zaira ya Kinabii ya mwezi wa kumi na mbili mwaka huu.
Wasiliana na Mratibu wa Ziara hiyo Elibariki Minja katika simu nambari 0786205768, 0715 452730 na 0754 452730 kwa maelezo zaidi.

Mungu akubariki sana kwa kulichagua taifa la Israeli kwani ni funguo za baraka yako

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni