YESU NI JIBU

Jumapili, 4 Agosti 2013

HITIMISHO LA WIKI KUMI NA TATU ZA UREJESHO KATIKA VIWANJA VYA EAGT CITY CENTER

Hatimaye leo ni leo ambayo ni kilee cha  wiki 13  za urejesho katika kanisa la EAGT City Center mara baada ya maelfu ya waumini kumiminika za idi ya kufurika katika ukumbi wa PTA uliopo katika viwanja vya Mwalimu Julias Kambarage Nyerere jijini DSM

Akielezea juu ya wiki 21 za urejesho na ukombozi ambapo zitahitimika tarehe 29 decemba 2013 na ratiba za ibada hizo asubuhi muda wa saa kumi na mbili na nusu

Awali ya alisimama mwalimu Emilian Busara ambaye alifundisha juu ya somo la ujasiria mali na watu wengi walimsikiliza mwalimu kwa makini na kufahamu mambo mengi.

Watu wengi wameanza kufunguliwa mara baada ya ibada ya kwanza kuanza na watu wengi wamefurahia sana kufunguliwa katika matatizo yao mbalimbali mara baada ya kuingia katika ukumbi wa PTA



Hapa mtumishi wa Mungu mchungaji Floriance Katunzi akisisitiza katika ibada ya kusifu na kuabudu



Huyu ni mwimbaji wa nyimbo za injili ni kiongozi wa kanisa la EAGT City center akihudumu katika madhabahuni ambapoa liimba wimba wa kuabudu

Huyu ni mwimbaji wa nyimbo za injili anayejulikana kwa jina la Neema Gaspa ambaye anatamba kwa kibao kinachofahamika kwa jina la Ni Shujaa.Mwimbaji huyu pia anategemea kuzindua albamu yake katika ukumbi wa Blue Peal Ubungo Plaza tarehe 1septemba mwaka huu ambapo wakali mbalimbali wa nyimbo za injili watamsindikiza katika uzinduzi huo.
Neema akihojiwa katika studio namba mbili ya WAPO Radio wakati ikirusha matangazo moja kwa moja kutoka katika kanisa la EACT City center viwanja vya sabasaba ukumbi wa PTA.


Hapa akiwajibika madhabahuni huku waumini mbalimbali wakimuunga mkono katika ukumbi huo.


 Neema akishirikiana na wacheza shoo wake katika madhabahu ya EAGT



Hapa sasa kazi  ipo wanavyowajibika madabahuni Neema na kundi lake


Mtangazaji wa WAPO RADIO FM Bi Angelina Lukindo  kulia mwenye miwani akiimba na kusifu ndani ya ukumbi wa PTA uliopo ktk viwanja vya saba saba



Wanakwaya wa kwaya majestic singers wakiimba katika ibada



Charles naye ni mmoja wa wwaimbaji  huduma ya EAGT CITY CENTER(EAGT)
Huyu ni mwimbaji Alex Anania ambaye naye ni mshirika wa kanisa la EAGT city center ambaya anawimbo wake unajina Tumevuka salama.

 Hawa ni baadhi ya waumini ambao wamemiminika katika ukumbi wa PTA kukutana na Mungu katika ibada ya kuhitimisha wiki 13 za urejesho.

Huyu ni mama ambaye ni miongoni mwa waumini waliofurika katika ukumbi wa PTA wakimsifu na kumwabudu Mungu



Katika ibada hiyo ya kipekeee watoto hawakuwa nyuma katika kusifu na kushangilia pamoja na waumini wengine.


Hivi ndivyo ukumbi ulivyo furika maelfu wa waumini ambao wamefunguliwa katika matatizo mbalimbali na vifungo vya Ibilisi .

Hapa utaona jitihada mbalimbali zinafanyika kila mmoja akifanya juhudi za kupata picha kwenye simu yake ya kiganjani.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni