YESU NI JIBU

Jumatatu, 18 Machi 2013

TAMASHA LA WAKONGWE LAFANA DAR

 Kongamano la wakongwe ambalo limefanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar limekuwa la ajabu sana.
Katika tamasha hilo wameshiriki waimbaji mbalimbali wakongwe ambao waliimba nyimbo ambazo waliziimba na zilivuma wakati wa zamani sana




Mgeni rasmi katika tamasha la wakongwe ndugu Patric Chokara,akizungumza katika tamasha hilo amesema ni vyema waimbaji wakongwe waenziwe maana kazi walizofanya ni njema.


Ndugu Emanuel akiwa na mke wake ambaye ndiye mratibu wa tamasha akizungumza katika tamasha la hilo wakongwe amesema kuwa amekutana na vikwazo mbalimbali wakati akitangaza tamasha hilo



 Mke wa waziri wa uchukuzi Linna Mwakiembe akikabidhi cheti kwa mwimbaji mkongwe wa injili

 Waimbaji wa kundi la New life bendi wawajibika jukwaani.



 Abednogo akipapasa kinanda ktk tamasha la wakngwe


Mchungaji Amon Kilahiro akifurahia jambo na mwimbaji wa New Life Band ndugu Abednego katika ukumbi wa Diamond Jubilee

Waimbaji wakongwe wakifuatilia kwa makini tamasha la wakongwe.


Upendo Nkone akifurahia tamasha la wakongwe.

Mchungaji Safari akiimba jukwaani katika tamasha



Linna Mwakyembe akimkabidhi pastor Safari cheti
 Mwimbaji Mwalukasa akionesha cheti aliyopokea katika tamasha la wakongwe.



Kiongozi wa Messengers bend ndugu Noeli akionesha cheti kushoto mke wa waziri wa uchukuzi Linna Mwakyembe.
 Mchungaji Amon na Upendo Kilahiro akiwa na picha ya pamoja na mtoto wao katika tamasha la wakongwe.
Waimbaji wakongwe wakiwa katika picha ya pamoja katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Mchungaji Olgenesi akiwepo kwenye jukwaa baada kupokea cheti.
Mkongwe wa nyimbo za injili mzee makasy wakihojiwa na mwandaaji wa kipindi cha televisheni cha Clouds.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni