YESU NI JIBU

Jumanne, 30 Novemba 2021

WANAOHARIBU UBORA WA MAZIWA KUCHUKULIWA HATUA.

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani Sara Msafiri akizungumza na wadau wa Maziwa wakati alipofungua mafunzo ya siku mbili yaliyofanyika kwa wafugaji wa Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani. Wafugaji na wauzaji wa maziwa wamewaonya na kaimu mkuu wa kitengo cha uthibiti ubora wa shirika la viwango nchini (TBS) Baraka Mbajige kuacha tabia ya kuweka maji kwenye maziwa kwa sababu ni kinyume cha sheria. Alisema hayo katika mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na TBS kwa wafugaji wa Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani ambapo adhabu ya mfugaji anayeweka maji kwenye maziwa ni faini ama kufungiwa. Kitendo cha kuweka maji kwenye maziwa ni kinyume cha sharia na taratibu maana unapoteza uhalisia wa kile unachowaulizia walaji. Kwa upande wake Meneja Utafiti wa Mafunzo Sudi Mwanansela alisema kuwa TBS wamefanya mafunzo hayo ikiwa na lengo la kuwapa elimu ya namna ya usindikaji, ubebaji Ili kuweza kuyapandisha thamani sokoni na kwa mlaji kwa ujumla. "Tutakuwa na mafunzo kwa siku mbili. hapa Kibaha ambapo tutajifunza kwa kutoa elimu na pia tutakwenda kuwafundisha kwa vitendo ambapo tutakwenda kuwatembelea kwenye maeneo ya na kuona namna wanavyofuga na kung'amua changamoto wanazozipitia Ili tuone namna ya kuweza kuwasaidia kuzitatua" alisema Mwanansela. Mafunzo hayo yalifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Sara Msafiri ambapo amewataka wafugaji hao kuondoka na maazimio ya kukua katika sekta hiyo ya maziwa na kuwataka wakati ujao waweze kuandaa Kongamano kubwa ambapo pia waweze kuwaita wadau wakubwa wakiwemo Idara ya Lishe ambao wataweza kujadili kwa kina suala la udumavu na umuhimu wa unywaji maziwa.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni