YESU NI JIBU

Jumatatu, 29 Juni 2015

TGNP IMESEMA HAIPO TAYARI KUSHIRIKIANA NA WALE VIONGOZI AMBAO HATAWAHAKIKISHIA WANAWAKE NA WALEMAVU HAKI ZAO.



Mtandao wa jinsia Tanzania TGNP  umeeleza kuwa hauko tayari kuwaunga mkono wale watu wanaohitji kuwa viongozi wa Taifa endapo hawatawahakikishia wananchi kuwa watatetea haki zote za  wanawake na walemavu.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa TGNP LILIAN LIUNDI Wakati akiongea na waandishi wa habari katika warsha ya kuwajengea uwezo wa kuandika habari mbalimbali zinazilohusiana na masuala ya uchaguzi pamoja na bajeti kwa mrengo wa kijinsia.
Liundi amesema kuwa wanachotaka ni kuona kuwa
viongozi watakaoingia madarakani wanakuwa na tamko mahususi linalolenga kumtetea mwanamke na kumuondoa katika matatizo mbalimbali yanayomkabili yakiwemo yale ya kuwa na haki ya kumiliki rasilimali pamoja na haki nyingine anazopaswa kupata.

Naye mkurugenzi wa bodi TGNP VICENCIA SHULE ameeleza kuwa ili nchi iweze kuimarika kimaendeleo serikili haina budi kuweka usawa wa kijinsia katika bajeti.
Ameeleza katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wagombea wengi wanatumia kiwango kikubwa cha rasilimali wakati wanapokuwa wanatangaza nia hivyo kukatisha tamaa watu

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni